Cambridge IGCSE Swahili 0262 — 2024 May/June Paper 1 · Variant 0
0262/10/M/J/24 · 60 marks · ≈68 min
The question paper and its mark scheme, free to read here and free to download. This is Cambridge’s own paper, exactly as it was sat.
Question paper16 pages
















Mark scheme
No mark scheme is in the library for this paper.
Paper as text
Question paper, page 1
This document has 16 pages. Any blank pages are indicated. [Turn over Cambridge IGCSE™ SWAHILI 0262/01 Paper 1 Reading and Writing May/June 2024 2 hours You must answer on the question paper. No additional materials are needed. INSTRUCTIONS ● Answer all questions. ● Use a black or dark blue pen. ● Write your name, centre number and candidate number in the boxes at the top of the page. ● Write your answer to each question in the space provided. ● Do not use an erasable pen or correction fluid. ● Do not write on any bar codes. ● Dictionaries are not allowed. INFORMATION ● The total mark for this paper is 60. ● The number of marks for each question or part question is shown in brackets [ ]. * 7 3 5 8 8 3 2 9 0 3 * DC (SL) 332412/3 © UCLES 2024
Question paper, page 2
2 0262/01/M/J/24 © UCLES 2024 Zoezi 1 Soma kifungu kifuatacho kuhusu miti ya mibuyu halafu jibu maswali yanayofuata. Mibuyu ni miti inayoheshimiwa sana katika bara la Afrika. Jamii nyingi huiita ‘miti ya maisha’ kwani ina faida nyingi sana ambazo huboresha maisha. Miti hii humea zaidi katika maeneo yenye ukame au pale ambapo hakuna mvua nyingi. Asili hasa ya mibuyu ni nchi zilizo kusini mwa bara la Afrika. Mibuyu pia imehusishwa na utambulisho kwani watu wengi husema kwamba mibuyu ni miti ambayo ina hadhi ya utambulisho wa Waafrika. Sijawahi kusikia mtu akipanda mbuyu kwenye bustani yake binafsi ingawa watu huipanda kwenye mashamba ambayo yana ardhi kavu iliyojaa mchanga. Juzi nilisoma kwamba kuna mibuyu nchi ya Hispania na sikutegemea kabisa mti huu kuota Ulaya. Zamani mibuyu ilijiotea tu yenyewe kutokana na kupukutika kwa mbegu zake. Ni kawaida kusikia watu wakisema kwamba hawajawahi kuona umbile la mti kama mbuyu. Huu ni mti ambao, unapotazamwa kwa mbali, unaonekana kama umegeuzwa juu chini, chini juu. Mimi ninadhani taswira hii hupotea pale mbuyu unapokuwa na majani pamoja na maua yake meupe. Matawi huonekana kama mizizi pale majani yake yanapopukutika. Watu hushangaa kwamba mbuyu una uwezo wa kuhifadhi maji mengi sana ndani ya shina lake pana. Nilisoma mahali kwamba mibuyu mikubwa inaweza kuhifadhi maelfu ya lita za maji. Uwezo huu unatokana na ukweli kwamba shina la mbuyu huwa na uwazi mkubwa na mpana sana kwa ndani. Ingawa katika historia ya utamaduni wetu, thamani yake hasa imetokana na uwezo wa mibuyu kuishi kwa maelfu ya miaka. Tulisoma kwenye darasa letu la historia kwamba hapo zamani viumbe hai waliishi ndani ya mashina ya mibuyu na walikuwa na nafasi ya kutosha. Katika sehemu zingine mashina ya mibuyu yalitumika kama jela. Pia jamii za wachungaji zilifugia mifugo yao na hivyo kutumia shina la mbuyu kama zizi. Tunda la mbuyu ni chanzo cha virutubisho vizuri kwa mwili wa binadamu na hutumiwa kwa matibabu. Mimi nimebahatika kuishi Afrika Kusini ambako ni rahisi kupata matunda ya mabuyu na kutengeneza sharbati yenye ladha ya malimao. Licha ya gharama ya kupata mbegu za mbuyu mtu anapokuwa nje ya bara, bado watu hupenda kuzitumia ili kuongeza nguvu na kutibu magonjwa kote duniani. Wapishi huchanganya tunda hilo pamoja na maji na sukari halafu hunywa. Pia wataalamu husaga mbegu na kutengeneza mafuta ambayo ni mazuri kwa mwili, hasa kama mtu akipakaa kwenye nywele au hata ngozini. Sijawahi kusikia mtu akipika kwa mafuta ya ubuyu.
Question paper, page 3
3 0262/01/M/J/24 © UCLES 2024 [Turn over 1 Jina mbadala la mbuyu ni? … [1] 2 Ushauri gani unatolewa kwa wanaotaka kupanda mbuyu? … [1] 3 Habari gani imemshangaza mwandishi? … [1] 4 Jambo gani linafanya mbuyu kuwa na taswira ya ajabu? … [1] 5 Umuhimu wa kijadi wa mbuyu ni? … [1] 6 Aina gani za malazi yamehusishwa na mibuyu? Taja aina mbili. … … [2] 7 Kikwazo cha kutumia ubuyu ng’ambo? … [1] [Jumla: 8]
Question paper, page 4
4 0262/01/M/J/24 © UCLES 2024 Zoezi 2 Wanafunzi wanne wanaelezea kuhusu mapishi. A Roza Pasaka ya mwaka huu nilipika samaki mtamu sana. Nilimjaza viungo mbalimbali na limau pamoja na pilipili kidogo. Si kawaida yangu kuingia jikoni na kupika kwani nipo mwaka wa mwisho wa shule na nitaanza kusoma chuo kikuu mwaka ujao na sitakuwa na jiko. Ninapoamua kupika basi mimi huchagua upishi wa kuvutia ambao kila mtu ataukumbuka kwa muda. Pia kwa sababu mimi hupenda kupika vyakula ambavyo hatuli mara kwa mara, ninahitaji kuenda kwenye duka la vyakula maalumu lililo karibu na kwetu ambapo hununua mahitaji yangu yote. Ninapoingia jikoni kila mtu hufurahia wakijua chakula kitakuwa kitamu, na mimi hustarehe kuwa jikoni. Sikukuu nyingine labda nitapika biringanya ambazo nitazioka pamoja na vitunguu na jibini. Ninafikiri kuna umuhimu kwa familia yangu kupunguza kula nyama na samaki. B Mikeli Dada yangu ameanzisha kipindi cha mapishi kwenye mtandao wa kijamii na bibi yetu ndiye mwalikwa mahsusi wa kipindi hicho. Mara nyingi vyakula anavyopika vinakuwa hata havina ladha nzuri lakini bahati nzuri watazamaji wake hawajui, wanatazama picha na kufikiri kwa vile chakula kinaonekana kizuri basi kina ladha. Mimi siamini kabisa wapishi wa mitandaoni kwa sababu ninajua wengine wanajidai tu. Nimejifunza kupika mwenyewe tu kwa kuwaangalia watu tofauti wakipika jikoni kwetu na ninahisi upishi ni ujuzi muhimu kuwa nao. Hakuna mtu anayezaliwa akiwa mjuzi wa upishi, inabidi kujitahidi kupika mara kwa mara. Siwezi kupika vyakula vinavyochukua muda mrefu na vyenye kuhitaji hatua nyingi mno. Ninapendelea vyakula vya haraka. C Micha Nimejifunza kupika mtandaoni kwa kutazama video za wapishi na sasa nimekuwa hodari hadi mimi mwenyewe hutunga mapishi yangu. Kwa vile nilijifunza mitandaoni mimi hupima kila kitu ambacho ninakitumia kwenye mapishi. Hii ni tofauti na bibi yangu ambaye hana kipimo kabisa. Kama nikikosa viungo vya kuweka kwenye chakula basi mimi hutumia viungo mbadala. Kwa mfano, nikikosa vitunguu maji ninaweza kutumia thomu. Nilipoanza kujifunza kupika nilifanya makosa mengi na kulazimika kutupa vyakula. Nilijaribu kufuata hatua zote za wapishi mtandaoni lakini chakula hakikutokea kama chao. Nahisi kupima mahitaji kabla ya kupika ni kujichosha, hasa kwa vile sina blogu ya mapishi hivyo makosa yangu hayaonekani na watu huko nje. Dada yangu aliniambia kwamba makosa ni elimu kwani husaidia mtu kujifunza vizuri. D Farhiya Mwezi huu wa Ramadhani nimejifunza kupika vyakula vingi kwani bibi yetu alikuja kukaa na sisi. Amenifundisha mapishi ayapendayo ya zamani na kunishauri kwamba urafiki hushamiri iwapo watu wanapika pamoja. Mama yangu alishangaa kuniona nikiingia jikoni kwani niligoma kabisa hapo awali. Kilichonivutia hasa ni hadithi za bibi tulipokuwa jikoni; ninafikiri sasa nimekuwa mwanahistoria na mwaka ujao nitaanzisha blogu ya mapishi ambapo nitaelezea mapishi tofauti, historia za vyakula na sehemu vyakula vinapopikwa. Tena hii inaweza kuwa ajira yangu. Kuna vyakula bibi yangu amevisifia ambavyo kamwe sitakubali kuvionja, mfano mmoja ni wadudu ambao hutoka ardhini pale mvua inaponyesha. Yeye anasema wao waliwakamata na kuwakaanga halafu baadaye waliwaweka ndani ya mchuzi. Ninahisi bora nibaki na njaa kuliko kula hao wadudu hata kama ni watamu kiasi gani.
Question paper, page 5
5 0262/01/M/J/24 © UCLES 2024 [Turn over Soma taarifa (8–16) zifuatazo. Weka alama ya tiki (✓) kwenye kisanduku kuonyesha aya (A–D) inayohusiana na kila taarifa. Kuna mfano mmoja hapa chini. Mfano Nani … hupika kwa nadra kwa sababu anasoma A ✓ B C D 8 anasifu mapishi yake na kuyaamini sana A B C D [1] 9 havutiwi na wazo la kuchukua muda mrefu kupika A B C D [1] 10 anazungumzia hisia hasi ya kula mapishi fulani A B C D [1] 11 anatoa pendekezo la kupika mapishi ukosapo mahitaji A B C D [1] 12 amepata uelewa uliovuka mpaka wa mapishi A B C D [1] 13 haamini wataalamu wa mitandaoni A B C D [1] 14 amepewa ushauri kuhusiana na tatizo kwenye upishi A B C D [1]
Question paper, page 6
6 0262/01/M/J/24 © UCLES 2024 15 anafikiria wakati ujao na kuuhusisha na chakula A B C D [1] 16 havutiwi na wazo la kufuata vipimo kwenye upishi A B C D [1] [Jumla: 9]
Question paper, page 7
7 0262/01/M/J/24 © UCLES 2024 [Turn over PLEASE TURN OVER FOR EXERCISE 3
Question paper, page 8
8 0262/01/M/J/24 © UCLES 2024 Zoezi 3 Soma makala yafuatayo kuhusu Mapambo ya Mazingira Asilia. Siku hizi kuna mtindo wa kuwa na nyumba zilizojaa vitu vilivyotoka kwenye mazingira asilia. Vitu hivi huweza kuwa mifupa iliyokauka, manyoya yanayong’aa na hata matawi ya miti tofauti. Mapambo haya huweza kuokotwa bustanini, barabarani au hata kwenye fukwe za bahari na pia huweza kununuliwa kwenye masoko ya mitumba na sehemu za sanaa ya maonyesho. Inasemekana kwamba kuvutiwa na mapambo yanayotokana na mazingira asili hakujaanza hivi karibuni; zamani watu walipenda kupamba kombe za baharini na walitumia pesa na muda wao kusafiri kuenda fukwe za mbali ili kuzipata kombe hizo. Athari moja ya matendo haya ni kupotea kwa vitu tofauti kwenye mazingira asilia. Wanafalsafa wanasema kwamba hamu ya kumiliki vitu vya asili ambavyo vimebadilika kwa kiasi kidogo sana kutoka karne moja hadi nyingine ni jambo la kawaida ingawa siku hizi kutokana na maisha ya kisasa ambapo watu huthamini usafi wa hali ya juu, mapenzi haya yamepungua. Bila shaka bado wapo watu ambao wana hamu ya kukusanya vitu ili wahisi kwamba wanaishi kwenye mazingira asilia, ingawa tabia hii inapungua sana kwa sababu ya kuwepo kwa hatari za afya kama vumbi na wadudu. Shilinde anakumbuka kwamba, alipokuwa mtoto alijaribu kuokota vijiti, mawe na manyoya ya njiwa, lakini mama yake alivitupa hivyo vitu kwani alitaka nyumba yao iwe safi kabisa. Alipokua, yeye alivutiwa sana na kutembelea majumba ya makumbusho. Aliwekeza pesa ili kutembelea makumbusho na alipokuwa huko alihisi raha na kujiona kama amezungukwa na mazingira asilia, hasa kwa sababu kulikuwa na vitu kutoka sehemu tofauti duniani. Maishani mwake kote Shilinde amekuwa na hamu ya kuwa na nyumba ambapo angeweza kuwa na mazingira asilia. Hivi sasa katika nyumba yake mwenyewe ameweza kufanikiwa. Shilinde amepaka kuta zake ndefu rangi ya machungwa iliyokoza na ameipamba kwa vitu vilivyotoka kwenye mazingira. Mapambo yake ni matawi yenye vijiti ambayo aliyakausha mwenyewe pamoja na mawe yenye maumbo tofauti. Anapokuwa nyumbani anahisi kama yupo kwenye jumba la makumbusho. Anasema kwamba hata harufu ya nyumba yake ni kama ile ya kwenye makumbusho; jambo linalompa furaha kubwa kwani ameweza kuleta mazingira ya nje, ndani ya nyumba yake. Mama yake ambaye alimwiga bibi yake kwa kila kitu humwambia ‘ni kosa kuchukua vitu kwenye mazingira bila ruhusa maalumu, wewe si mtaalamu, bora ungepanda maua kwenye vyungu kwani yangependeza zaidi’. Tofauti na Shilinde, Lilian anapenda kuishi kwenye nyumba yake ndogo na nadhifu ambayo haina mapambo kabisa. Nyumba yake ina kuta nyeupe na madirisha ya wastani. Yeye alifanya maamuzi ya kuishi kwenye nyumba hiyo ndogo kwa sababu hapendi makorokoro kabisa. Anasema yeye aliamua kuishi katika nafasi ndogo kwa makusudi kwani kunamlazimisha kutupa vitu ambavyo hana lazima ya kuwa navyo. Kama akiwa hajatumia kifaa kwa zaidi ya miezi miwili basi yeye hukigawa au hukitupa. Vilevile, Lilian amejionea mwenyewe jinsi mapambo mengi ya asili huweza kuoza na kuwa na harufu mbaya. Tofauti na nyumbani, anapokuwa kazini, Lilian huzungukwa na makorokoro kutoka kwenye mazingira kwani yeye ni msanii anayetengeneza sanaa yake kwa kutumia magome ya miti kama mibuyu, vijiti ambavyo huvipinda na kuvinyoosha ili kuunda mapambo ya kuvutia na pia shanga. Lilian huuza vitu vyote hivi; kamwe havichukui nyumbani kwake. Lilian husema kwamba ni muhimu kwa wataalamu kama yeye kutengeneza mapambo asilia kwani wanafahamu vitu visivyofaa kuchukuliwa na vile ambavyo ni ruhusa kuchukua. Alipokuwa mtoto wazazi wake walikuwa na nyumba iliyojaa kila aina ya mapambo hadi kufanya watu washindwe kutembea kwa raha. Kila waliposafiri walinunua mapambo tofauti kama vitambaa na vinyago. Lilian alianza kutengeneza vidani kwa kutumia shanga zilizojaa nyumbani kwao na polepole akaanza kutumia vitu vingine hadi sasa amekuwa bingwa wa kutengeneza mapambo.
Question paper, page 9
9 0262/01/M/J/24 © UCLES 2024 [Turn over Andika maelezo mafupi chini ya vichwa vya habari (17–19) vinavyotokana na makala uliyoyasoma. [Jumla: 9] Katika zoezi 4, utatumia maelezo haya kutunga ufupisho. 17 Vitendo vya wazazi vilivyoshawishi upendeleo wa mapambo: • … • … • … [3] 18 Athari hasi za mapambo asilia: • … • … • … [3] 19 Uhusiano kati ya uchumi na mazingira asilia: • … • … • … [3]
Question paper, page 10
10 0262/01/M/J/24 © UCLES 2024 Zoezi 4 20 Sasa tunga ufupisho unaoonyesha faida na hasara za mapambo ya mazingira asilia. Unaweza kutumia maelezo yako mengine kutoka zoezi 3 ili kukusaidia. Ufupisho wako usizidi maneno 100. Tumia maneno yako mwenyewe kadiri iwezekanavyo. Utapata alama zisizozidi 4 kwa maudhui ya ufupisho wako, na alama zisizozidi 6 kwa lugha makini na sahihi. … … … … … … … … … … … … … … [Jumla: 10]
Question paper, page 11
11 0262/01/M/J/24 © UCLES 2024 [Turn over Zoezi 5 21 Umepata nafasi ya kutoa maelezo kuhusu tamasha ulilohudhuria hivi karibuni. Andika blogu itakayosomwa na watu duniani pote. Unapaswa kutaja: • aina ya tamasha • shughuli ulizofanya • changamoto za kuhudhuria tamasha. Blogu yako isizidi maneno 120. Utapata alama zisizozidi 3 kwa maudhui ya blogu yako, na alama zisizozidi 5 kwa mtindo na umakini wa matumizi ya lugha yako. … … … … … … … … … … … … … … [Jumla: 8]
Question paper, page 12
12 0262/01/M/J/24 © UCLES 2024 Zoezi 6 22 ‘Lazima sote tuanze kula mboga tu na kuacha nyama.’ Je, unakubaliana na wazo hili? Andika makala katika gazeti la shule ili kutoa maoni yako. Makala yasizidi maneno 200. Mboga zina virutubisho vyote tunavyohitaji na zinapunguza uchafuzi wa mazingira! Tumekula nyama kwa karne kadhaa, miili yetu inahitaji nyama! Unaweza kutumia maoni ya hapo juu, na pia ni lazima kutumia mawazo yako mwenyewe. Utapata alama zisizozidi 8 kwa maudhui ya makala, na alama zisizozidi 8 kwa mtindo na umakini wa matumizi ya lugha yako. … … … … … … … … … … … … … … … … … …
Question paper, page 13
13 0262/01/M/J/24 © UCLES 2024 … … … … … … … … … … … … [Jumla: 16]
Question paper, page 14
14 0262/01/M/J/24 © UCLES 2024 BLANK PAGE
Question paper, page 15
15 0262/01/M/J/24 © UCLES 2024 BLANK PAGE
Question paper, page 16
16 0262/01/M/J/24 © UCLES 2024 Permission to reproduce items where third-party owned material protected by copyright is included has been sought and cleared where possible. Every reasonable effort has been made by the publisher (UCLES) to trace copyright holders, but if any items requiring clearance have unwittingly been included, the publisher will be pleased to make amends at the earliest possible opportunity. To avoid the issue of disclosure of answer-related information to candidates, all copyright acknowledgements are reproduced online in the Cambridge Assessment International Education Copyright Acknowledgements Booklet. This is produced for each series of examinations and is freely available to download at www.cambridgeinternational.org after the live examination series. Cambridge Assessment International Education is part of Cambridge Assessment. Cambridge Assessment is the brand name of the University of Cambridge Local Examinations Syndicate (UCLES), which is a department of the University of Cambridge. BLANK PAGE
What you needed in this session
Cambridge’s own grade thresholds for 2024 May/June, Paper 1 · Variant 0. A higher threshold means an easier paper — the bar moves with how the cohort did.