Cambridge IGCSE Swahili 0262 — 2022 May/June Paper 1 · Variant 0
0262/10/M/J/22 · 60 marks · ≈68 min
The question paper and its mark scheme, free to read here and free to download. This is Cambridge’s own paper, exactly as it was sat.
Question paper16 pages
















Mark scheme
No mark scheme is in the library for this paper.
Paper as text
Question paper, page 1
This document has 16 pages. Any blank pages are indicated. [Turn over Cambridge IGCSE™ DC (PQ) 303041/4 © UCLES 2022 SWAHILI 0262/01 Paper 1 Reading and Writing May/June 2022 2 hours You must answer on the question paper. No additional materials are needed. INSTRUCTIONS ● Answer all questions. ● Use a black or dark blue pen. ● Write your name, centre number and candidate number in the boxes at the top of the page. ● Write your answer to each question in the space provided. ● Do not use an erasable pen or correction fluid. ● Do not write on any bar codes. ● Dictionaries are not allowed. INFORMATION ● The total mark for this paper is 60. ● The number of marks for each question or part question is shown in brackets [ ]. * 5 6 0 3 1 7 3 0 8 6 *
Question paper, page 2
2 0262/01/M/J/22 © UCLES 2022 Zoezi 1 Soma kifungu kifuatacho kuhusu usafiri na halafu jibu maswali yanayofuata. Kuna aina nyingi za usafiri wa kila siku. Mtu anaweza kuendesha gari, kupanda basi au treni, kukodi teksi au kutembea kwa miguu. Inaonekana kwamba siku hizi watu wengi wanapenda sana kutembea au kupanda baisikeli. Zamani watu walipopanda baisikeli au kutembea walionekana kama fukara na hawana uwezo wa kununua gari au kulipia usafiri wa umma. Siku hizi watu wanaelewa kuwa magari yanaleta uchafuzi wa mazingira, na pia kuna sababu za kiuchumi kwani kutembea na kutumia baisikeli ni bure kabisa. Hata hivyo huku kwetu bado gari linaendelea kuwa muhimu kwani watu wengine huwa na familia kubwa inayojumuisha ndugu na jamaa tofauti, kwa hivyo ni lazima kuwa na usafiri madhubuti. Nilifanya utafiti pamoja na kaka yangu na tuligundua kwamba katika mji wetu, zaidi ya asilimia 50 ya watu hutumia baisikeli kama njia yao kuu ya usafiri. Kati ya hawa, wapo ambao hufanyia kazi zao kwenye baisikeli. Mfano mzuri ni wale wanaouza madafu, mboga na matunda ambayo huyapakia kwenye baisikeli zao. Wao huwa na matenga makubwa yaliyojaa bidhaa na huzunguka mitaani huku wakiuza. Zaidi ya hapo, takriban asilimia 20 ya watu hutumia baisikeli mara moja moja ili kuenda kazini au shuleni. Pia kuna asilimia ndogo ya watu ambao hupanda baisikeli kwa ajili ya mashindano. Mimi ni katika watu walioshindana katika mbio za baisikeli zilizotoka Tanzania hadi Afrika ya Kusini. Sikuwa na nguo zinazotakiwa kwa ajili ya mashindano, kwani sikuwa na uwezo wa kununua mpya kwa sababu muhimu zaidi ilikuwa ni kupata baisikeli haraka. Ilibidi baba aninunulie baisikeli mpya ya mashindano. Ilikuwa ghali sana na alisema hataninunulia baisikeli nyingine kwa miaka kumi ijayo. Tulipofika Afrika ya Kusini nilishangaa kuona barabara maalumu za baisikeli. Niliporudi kwetu nilimhadithia mama yangu aliyewaambia ndugu zetu ‘Salha alipokuwa kule sikuwa na wasiwasi wowote wa ajali za barabarani na sasa mimi nitakwenda naye mwaka ujao’. Mimi nitafurahi kuwa na mama yangu katika mashindano lakini ninahisi nitalazimika kuendesha polepole ili nisimwache nyuma. Yeye ameshanunua taa mpya ambazo amezibandika nyuma na mbele ya baisikeli yake. Pia amenunua mnyororo madhubuti wa kuifungia baisikeli yake ili isiibiwe. Ningefurahia zaidi kama kaka yangu angekubali kuja kwani ni yeye aliyenifundisha kuendesha. Aliwaambia rafiki zake, ‘kamwe sikutegemea kwamba Salha angeenda hadi Afrika ya Kusini kwa baisikeli, safari ndefu na hatari’!
Question paper, page 3
3 0262/01/M/J/22 © UCLES 2022 [Turn over 1 Kwa nini watu wanaendesha baisikeli sasa? Taja sababu mbili. (i) … [1] (ii) … [1] 2 Usafiri wa gari unawavutia watu gani? … [1] 3 Matenga yana umuhimu gani kwa wauzaji? … [1] 4 Salha alipaswa kufanya nini ili kushiriki katika mashindano? … [1] 5 Kwa nini mama alibadili mawazo kuhusu usalama wa mashindano? … [1] 6 Kwa nini Salha angependelea kuingia kwenye mashindano na kaka na si mama? Taja sababu mbili. (i) … [1] (ii) … [1] [Jumla: 8]
Question paper, page 4
4 0262/01/M/J/22 © UCLES 2022 Zoezi 2 Wanafunzi wanne wanaelezea kuhusu chakula na mazoezi kwa afya bora. A Roza Afya njema inategemea sana chakula na mazoezi. Mimi ninakula lishe bora yenye virutubisho vingi. Ni kawaida yangu kuamka mapema sana na kufanya mazoezi. Zoezi ninalolipenda hasa ni kuruka kamba. Baada ya hapo hunyoosha viungo vyangu huku nikiwa nimejilaza sakafuni. Ninakula karibu kila kitu. Sidhani kama ningefaa kuwa daktari wa lishe kwa sababu sichagui vyakula, muhimu kiwe kinajenga mwili. Leo asubuhi nilikunywa uji na matunda, mchana nilisonga ugali na kitoweo kilikuwa maharagwe. Usiku nitakula wali na mboga mboga. Pia nyakati za jioni huwa ninapenda kutembea mtaani kwangu. Kwa njia hii ninaweza kufanya mazoezi mara mbili kwa siku na pia huwasalimia majirani zangu; labda siku moja nitajenga urafiki nao. Pia nimegundua kwamba ninapofanya mazoezi au kutembea, huwa ninasahau matatizo yangu yote na hujihisi mwepesi kabisa. B Juma Nilipokuwa shule nilipenda sana kuruka kamba. Tena niliipenda ile michezo inayohusu kamba ambapo mtu mmoja huwa kati na huruka wakati wengine wameshikilia pande zote mbili. Siku hizi siruki tena, ila ninanyanyua vyuma vizito. Jana usiku nilinyanyua vyuma vilivyokuwa na kilo 150. Misuli yangu imefura sana na ukiniona tu unajua kwamba mimi ni mtu wa mazoezi. Mimi sifanyi mazoezi kupumzisha akili, huyafanya ili nizidi kujivunia mwili wangu. Chakula ninachopendelea ni kuku na wali tu, kwani vyakula hivyo hujenga misuli. Mimi inapowezekana situmii vyakula vyenye sukari na mafuta. Watu huniuliza kwa nini sikimbii kwa mfano kwenye marathoni. Ukweli ni kwamba mwili wangu ni mzito, si kwamba sipendi kukimbia, la, mimi siwezi kukimbia ingawa nina nguvu sana. Zaidi ya kunyanyua vyuma, mimi hupenda kuzurura kwenye barabara karibu na nyumbani kwangu ambapo majirani wote wananijua na wanapenda kuniangalia nikipita, ingawa hawanisogelei. C Safia Mimi ninapendelea zaidi vyakula vyenye rangi rangi na vinavyovutia. Matunda ninayokula ni machungwa na mazambarau tu. Mboga zangu kuu ni mchicha na biringani. Mimi sili nyama wala samaki. Pia sili mayai na maziwa. Mama yangu ana wasiwasi kwamba kuna virutubisho ambavyo ninavikosa kwenye lishe yangu. Huwa ninamhakikishia kwamba huo si ukweli. Mimi nitasomea kuwa mwanasayansi wa lishe kwa hivyo ninajua ninachokifanya. Zoezi langu kuu ni lile la kunyoosha viungo. Ninapenda kujinyoosha hadi misuli yangu inasikia raha. Zoezi ambalo halinivutii kabisa ni lile la kunyanyua vyuma. Sioni maana ya kufanya hivyo ili kuonekana kuwa umejenga misuli lakini mwili haushituliwi kwa zoezi kama la kukimbia, kuruka kamba au kuogelea. Zamani nilipenda sana kucheza mpira wa mguu, tena nilikuwa mwanachama wa timu ya kandanda, lakini niliteguka na sikucheza tena ingawa sikosi kutazama mechi za timu yangu. D Luka Mimi ni mpenzi wa mpira wa miguu. Ninapenda sana kutazama michuano na pia kucheza. Siku hizi nimejiunga na timu ya vijana wenzangu na hucheza mpira na majirani zangu. Kwa njia hii tumejuana na kuwa marafiki. Uzuri wa mpira wa miguu ni kwamba sihisi kuchoka hadi inapofika mwisho wa mechi. Na hapo ninagundua kwamba nimeweza kukimbia masafa marefu pale uwanjani. Wenzangu wengi wanapenda kunyanyua vyuma vizito. Kwa mfano wengine hubeba hadi kilo 150. Lakini mimi sivutiwi kabisa na zoezi hilo. Kitu muhimu kwangu ni chakula. Mimi ninapenda sana chai na mkate asubuhi, mchana ninakula kilichopikwa nyumbani. Leo ilikuwa wali, nyama na maharagwe. Pia ninakula matunda tofauti na mboga. Mara moja moja pia hupenda kula vitafunio vya sukari kama kashata na visheti. Ninafikiri maishani ni muhimu kutojinyima.
Question paper, page 5
5 0262/01/M/J/22 © UCLES 2022 [Turn over Soma taarifa (7–15) zifuatazo. Weka alama ya tiki (✓) kwenye kisanduku kuonyesha aya (A–D) inayohusiana na kila taarifa. Kuna mfano mmoja hapa chini. Mfano Mwanafunzi yupi … anaamini watu wale vyakula wanavyovitaka? A B C D ✓ 7 anaruka kamba sasa? A B C D [1] 8 anajali zaidi jinsi anavyoonekana? A B C D [1] 9 ni mwanachama wa timu ya kandanda? A B C D [1] 10 amejenga urafiki na majirani? A B C D [1] 11 anachagua chakula mno? A B C D [1] 12 anaamini mazoezi hupumzisha akili? A B C D [1] 13 anapenda zoezi la kuinua uzito? A B C D [1]
Question paper, page 6
6 0262/01/M/J/22 © UCLES 2022 14 kukimbia ni changamoto kwake? A B C D [1] 15 ataweza kuwasaidia watu kuboresha lishe zao? A B C D [1] [Jumla: 9]
Question paper, page 7
7 0262/01/M/J/22 © UCLES 2022 [Turn over BLANK PAGE
Question paper, page 8
8 0262/01/M/J/22 © UCLES 2022 Zoezi 3 Soma makala yafuatayo kuhusu mafunzo nyumbani. Mwanzoni mwa mwaka wazazi walipewa nafasi ya kuwafundisha watoto wao nyumbani kwa ajili ya utafiti mpya kuhusu elimu. Kwa kipindi cha miezi mitatu, vyumba viligeuzwa kuwa madarasa. Wanafunzi walitumia vitabu vya mazoezi na mitandao tofauti kufanya kazi zao za shule. Walimu wengi walisikika wakisema ‘sasa kazi ya kufundisha imekuwa masaa 24 kwani wanafunzi wanatarajia kujibiwa hoja zao kutwa kucha, hatupumziki!’ Kwa wanafunzi, hali ilikuwa tofauti. Mwanzoni wengi walihisi itakuwa likizo tu. Wangeweza kusoma huku wakiwa vitandani mwao, tena wangejivalia nguo zao za kulalia. Wengi walifikiri wangeweza kupoteza muda kwenye mitandao ya kijamii wakidurusu majukwaa tofauti. Kiujumla wazazi walikuwa na wasiwasi kwamba watoto wangeweza kupotea njia kwa kutumia mitandao kwa muda mrefu na vibaya, hasa kwa kutazama video za kipuuzi. Pia walikuwa na hofu kwamba watoto wangepata tabia za kibinafsi za kutojali familia zao na kujali watu baki huko mitandaoni. Zaidi ya hapo, wengine walihofia kushindwa kuwasaidia watoto wao pale walipokwama masomoni. Baada ya miezi mitatu ya kukaa nyumbani, mawazo yamekuwa tofauti. Kuna wanafunzi ambao bado wanafurahia kusoma wakiwa nyumbani na kuna wengine ambao hawapendi kabisa. Kurwa anaishi Dar es salaam pamoja na wazazi wake. Utafiti ulipoanza Kurwa alidai kwamba hakutumiwa kazi yoyote na shule yake. Alionekana kama aliyekuwa likizoni. Baba yake alijiuliza kwa nini Kurwa alikuwa hafanyi kazi yoyote. Ilipofika wiki ya tatu, aliwasiliana na shule na kutaarifiwa kwamba walimu walifanya jukumu lao la kuwasiliana na mwanafunzi wao kwa kutumia simu au barua pepe lakini hakuwajibu. Baba akafahamishwa kwamba itabidi Kurwa aanze kusoma kwa kutumia mtandao. Ilipangwa kwamba shule ingemtumia kazi na walimu walipaswa kusahihisha kazi zake. Baba yake aliamua kumnunulia kompyuta na kuiweka chumbani kwake ili Kurwa aweze kufanya kazi kwa utulivu. Alimwambia mama yake Kurwa, ‘sasa mtoto atajifunza kujitegemea na kufanya utafiti wake mwenyewe’. Mama yake alihisi mtoto kujifungia si wazo zuri kwani angepoteza muda mwingi kucheza kwenye mitandao tofauti, ‘mimi siamini kumwachia tu mtoto, pia atakuwa mpweke sana’. Kurwa aliahidi kwamba atakuwa anatoka chumbani kila baada ya saa moja au mbili ili kumtuliza mama kwa kuzungumza naye kuhusu mambo tofauti. Zakia anaishi Moshi pamoja na mama yake. Mwanzoni mwa utafiti alikuwa na hofu kwamba, kwa kuwa nyumbani, mama yake angemtegemea yeye kufanya kazi zote za nyumbani. Alifurahi alipoona kwamba shule ilimpa kazi za kufanya katika vitabu vyake na pia mtandaoni. Kwa hivyo tangu siku ya kwanza alipokuwa nyumbani Zakia aliamka mapema na kufanya kazi zake za shule na mama hakumwambia kitu kuhusu kusaidia kazi za nyumbani. Kwa kawaida ilimchukua takriban saa tatu kumaliza kazi zote. ‘Ni ajabu, mimi mwenyewe niliamua kuingia jikoni baada ya masomo yangu na nikajifunza kuoka keki na kupika vyakula tofauti. Tena nilianza kutafuta vyakula vya kimataifa na kuvipika. Baada ya mapishi nilisafisha jiko na kumsaidia mama’. Mama hucheka na kusema ‘nilijua tu atasaidia nyumbani kwani Zakia ni mtoto mwenye nidhamu kwa hivyo nilimwacha aamue mwenyewe pale alipokuwa tayari’. Yeye amefurahia kuweza kuzungumza mengi na Zakia ingawa amegundua kwamba motisha ya kusoma mwenyewe imekuwa ikipungua na ile ya kuwa na mama imezidi. Aliporudi shule Zakia alisikitika kurudi darasani. Ingawa alipokuwa nyumbani alilazimika kutumia simu ya mama yake kusomea kwani mama yake hakuwa na uwezo wa kumnunulia kompyuta, lakini kuwa na mama kulimpa faraja kubwa. Alikuwa na hamu ya kuendelea kusoma nyumbani. Kurwa alifurahia sana kurudi shule kwani aliwakumbuka sana rafiki zake na hata walimu. ‘Sikupenda jinsi mtandao ulivyokuwa hauna uhakika hasa kiungo cha intaneti kilipotea; kwa kweli kusoma uso kwa uso ni bora zaidi!’ Mama yake aligundua kwamba tatizo halikuwa matumizi ya muda mrefu ya kompyuta; ‘tatizo nililoliona ni kwamba Kurwa alikosa motisha ya kusoma na alikuwa na hamu kubwa ya kuwa na wenziwe’.
Question paper, page 9
9 0262/01/M/J/22 © UCLES 2022 [Turn over Andika maelezo mafupi chini ya vichwa vya habari (16–19) vinavyotokana na makala uliyoyasoma. 16 Wajibu wa walimu: • … • … [2] 17 Faida za kusoma nyumbani kulingana na wazazi: • … • … • … [3] 18 Tofauti za wazazi wa Zakia na Kurwa: • … • … [2] 19 Matokeo ya utafiti ambayo wanafunzi hawakuyategemea: • … • … [2] [Jumla: 9] Katika zoezi 4, utatumia maelezo haya kutunga ufupisho.
Question paper, page 10
10 0262/01/M/J/22 © UCLES 2022 Zoezi 4 Makala ya zoezi 3 yanazungumzia mafunzo nyumbani. 20 Sasa tunga ufupisho unaolinganisha njia tofauti zilizochukuliwa na wazazi kuwajibika na mafunzo ya nyumbani. Unaweza kutumia maelezo yako mengine kutoka zoezi 3 ili kukusaidia. Ufupisho wako usizidi maneno 100. Tumia maneno yako mwenyewe kadiri iwezekanavyo. Utapata alama zisizozidi 4 kwa maudhui ya ufupisho wako, na alama zisizozidi 6 kwa lugha makini na sahihi. … … … … … … … … … … … … … … [Jumla: 10]
Question paper, page 11
11 0262/01/M/J/22 © UCLES 2022 [Turn over Zoezi 5 21 Umepata nafasi ya kutazama filamu mpya kwenye jumba la sinema karibu na nyumbani kwako. Andika blogu itakayosomwa na watu duniani pote. Unapaswa kutaja: • Sababu za kupenda kuenda sinema • Hali ya sinema ilivyo sasa • Mabadiliko utakayopenda kuona kwenye sinema Blogu yako isizidi maneno 120. Utapata alama zisizozidi 3 kwa maudhui ya blogu yako, na alama zisizozidi 5 kwa mtindo na umakini wa matumizi ya lugha yako. … … … … … … … … … … … … … … [Jumla: 8]
Question paper, page 12
12 0262/01/M/J/22 © UCLES 2022 Zoezi 6 22 Wahenga walisema: ‘pesa haziwezi kununua furaha’. Je, hayo ni kweli katika dunia ya leo? Andika makala katika gazeti la shule ili kutoa maoni yako. Makala yasizidi maneno 200. Mazuri ya dunia hayalipiwi! Sema utakalo, lakini unahitaji pesa kununua utakavyo! Unaweza kutumia maoni ya hapo juu, na pia ni lazima kutumia mawazo yako mwenyewe. Utapata alama zisizozidi 8 kwa maudhui ya makala, na alama zisizozidi 8 kwa mtindo na umakini wa matumizi ya lugha yako. … … … … … … … … … … … … … … … … … …
Question paper, page 13
13 0262/01/M/J/22 © UCLES 2022 … … … … … … … … … … … … [Jumla: 16]
Question paper, page 14
14 0262/01/M/J/22 © UCLES 2022 BLANK PAGE
Question paper, page 15
15 0262/01/M/J/22 © UCLES 2022 BLANK PAGE
Question paper, page 16
16 0262/01/M/J/22 © UCLES 2022 Permission to reproduce items where third-party owned material protected by copyright is included has been sought and cleared where possible. Every reasonable effort has been made by the publisher (UCLES) to trace copyright holders, but if any items requiring clearance have unwittingly been included, the publisher will be pleased to make amends at the earliest possible opportunity. To avoid the issue of disclosure of answer-related information to candidates, all copyright acknowledgements are reproduced online in the Cambridge Assessment International Education Copyright Acknowledgements Booklet. This is produced for each series of examinations and is freely available to download at www.cambridgeinternational.org after the live examination series. Cambridge Assessment International Education is part of Cambridge Assessment. Cambridge Assessment is the brand name of the University of Cambridge Local Examinations Syndicate (UCLES), which is a department of the University of Cambridge. BLANK PAGE
What you needed in this session
Cambridge’s own grade thresholds for 2022 May/June, Paper 1 · Variant 0. A higher threshold means an easier paper — the bar moves with how the cohort did.