Cambridge IGCSE Swahili 0262 — 2021 May/June Paper 1 · Variant 0

0262/10/M/J/21

The question paper and its mark scheme, free to read here and free to download. This is Cambridge’s own paper, exactly as it was sat.

← All Swahili papers

Question paper16 pages

Cambridge IGCSE Swahili 0262 2021 May/June Paper 1 · Variant 0 question paper, page 1 of 16
Page 1 of 16
Cambridge IGCSE Swahili 0262 2021 May/June Paper 1 · Variant 0 question paper, page 2 of 16
Page 2 of 16
Cambridge IGCSE Swahili 0262 2021 May/June Paper 1 · Variant 0 question paper, page 3 of 16
Page 3 of 16
Cambridge IGCSE Swahili 0262 2021 May/June Paper 1 · Variant 0 question paper, page 4 of 16
Page 4 of 16
Cambridge IGCSE Swahili 0262 2021 May/June Paper 1 · Variant 0 question paper, page 5 of 16
Page 5 of 16
Cambridge IGCSE Swahili 0262 2021 May/June Paper 1 · Variant 0 question paper, page 6 of 16
Page 6 of 16
Cambridge IGCSE Swahili 0262 2021 May/June Paper 1 · Variant 0 question paper, page 7 of 16
Page 7 of 16
Cambridge IGCSE Swahili 0262 2021 May/June Paper 1 · Variant 0 question paper, page 8 of 16
Page 8 of 16
Cambridge IGCSE Swahili 0262 2021 May/June Paper 1 · Variant 0 question paper, page 9 of 16
Page 9 of 16
Cambridge IGCSE Swahili 0262 2021 May/June Paper 1 · Variant 0 question paper, page 10 of 16
Page 10 of 16
Cambridge IGCSE Swahili 0262 2021 May/June Paper 1 · Variant 0 question paper, page 11 of 16
Page 11 of 16
Cambridge IGCSE Swahili 0262 2021 May/June Paper 1 · Variant 0 question paper, page 12 of 16
Page 12 of 16
Cambridge IGCSE Swahili 0262 2021 May/June Paper 1 · Variant 0 question paper, page 13 of 16
Page 13 of 16
Cambridge IGCSE Swahili 0262 2021 May/June Paper 1 · Variant 0 question paper, page 14 of 16
Page 14 of 16
Cambridge IGCSE Swahili 0262 2021 May/June Paper 1 · Variant 0 question paper, page 15 of 16
Page 15 of 16
Cambridge IGCSE Swahili 0262 2021 May/June Paper 1 · Variant 0 question paper, page 16 of 16
Page 16 of 16

Mark scheme

No mark scheme is in the library for this paper.

Paper as text

Question paper, page 1

This document has 16 pages. Any blank pages are indicated. Cambridge IGCSE™ SWAHILI 0262/01 Paper 1 Reading and Writing May/June 2021 2 hours You must answer on the question paper. No additional materials are needed. INSTRUCTIONS ● Answer all questions. ● Use a black or dark blue pen. ● Write your name, centre number and candidate number in the boxes at the top of the page. ● Write your answer to each question in the space provided. ● Do not use an erasable pen or correction fluid. ● Do not write on any bar codes. ● Dictionaries are not allowed. INFORMATION ● The total mark for this paper is 60. ● The number of marks for each question or part question is shown in brackets [ ]. DC (KS/FC) 212561/3 © UCLES 2021 [Turn over * 4 2 3 5 6 6 0 2 8 3 *

Question paper, page 2

2 0262/01/M/J/21 © UCLES 2021 Zoezi 1 Soma kifungu kifuatacho kuhusu mpagazi Wambui Chege na halafu jibu maswali yanayofuata. Wiki iliyopita nilisoma habari kuhusu Wambui Chege, Mkenya mwenye urefu wa wastani na nywele zilizosokotwa. Yeye ni miongoni mwa wapagazi wachache ambao ni wanawake wanaofanya kazi katika Mlima wa Kilimanjaro uliopo Tanzania. Anapokuwa kazini, yeye huvaa suruali na mabuti mazito. Shughuli wanazofanya wapagazi ni mojawapo kati ya zile zinazoingiza mamilioni ya fedha ili kukuza uchumi. Pia huduma wanayoitoa huonyesha sura bora ya nchi. Huduma hizi ni kama kuwapa maelfu ya wapandaji milima fursa ya kujishughulisha na zoezi la kupanda mlima bila ya kuwa na wasiwasi kuhusu mizigo yao kwani wapagazi huibeba. Wao ni wenyeji kwa watu wanaopanda milima. Wapandaji wengi huwa na ufahamu wa kimo kirefu, lakini hushangazwa na kasi ya upepo wa theluji na umati wa watalii wanaokabiliana nao. Wambui anakubaliana nao kwani katika mahojiano yake alisema kwamba mara ya kwanza alipoupanda Mlima wa Kilimanjaro alikata shauri kwamba kamwe asingetaka kurudi tena mlimani huko kutokana na sababu hizo. Lakini alipopokea mshahara uliokuwa mkubwa kuliko alivyotegemea akaamua kuendelea na kazi hii. Na hadi hivi sasa ameshaupanda mlima huo zaidi ya mara hamsini. Mwanzoni Wambui alichoka sana na hata alishindwa kutembea vizuri kwa maumivu, lakini sasa shida kubwa anayoiona ni ile ya watu wengi kumwambia kwamba upagazi ni shughuli ya wanaume, si ya wanawake. Wao wanahisi kwamba wanawake hawatakiwi kufanya kazi ngumu. Wambui hakubaliani na mawazo hayo. Alisema kwamba watu wote ni sawa. Yeye kama mpagazi anahitajika zaidi katika maeneo ambayo hayana barabara na anafanya kazi pamoja na wenzake kama waongozaji na wapishi ambao ni wanawake kwa wanaume. Waongozaji ndio viongozi wenyewe na wao hufanya maamuzi yote kuhusu safari. Kwa mfano, huamua muda wa kuanza safari. Wapishi hutayarisha milo pale wasafiri wanapofika katika kambi tofauti. Wambui alifafanua kwamba Mlima wa Kilimanjaro una kambi au vituo vikuu vitatu, navyo ni Mandara, Horombo na Kibo. Wambui alisema kutoka kituo kimoja hadi kingine wapandaji wanaweza kuchukua muda wa saa sita, au hata zaidi wakati wa jua la mchana. Kwa hivyo, mara nyingi waongozaji hufanya uamuzi wa kuukwea mlima gizani, hasa kutokea kituo cha Kibo kuelekea kileleni. Baada ya kusikiliza mahojiano ya Wambui nilibaini kwamba kazi wanayofanya wapagazi ndiyo hasa uti wa mgongo wa safari za milimani. Wao hubeba takribani kilo ishirini za vitu muhimu kama mahema, mablanketi, chakula, dawa na maji. Pia hubeba vifaa kama meza, viti na hata magodoro. Hivi sasa Wambui anafanya mafunzo yatakayomwezesha kuwa mwongoza watalii. Hiyo ndiyo ndoto yake.

Question paper, page 3

3 0262/01/M/J/21 © UCLES 2021 [Turn over 1 Kwa nini kazi ya upagazi ni muhimu kwa nchi? Taja sababu mbili. … … [2] 2 Mlima wa Kilimanjaro una changamoto gani zisizotegemewa? Taja changamoto mbili. … … [2] 3 Kitu gani kilimfanya Wambui asikate tamaa baada ya safari ya kwanza? … [1] 4 Tatizo kubwa linaloendelea kwa Wambui ni lipi? … [1] 5 Kwa nini waongozaji huanza safari wakati wa usiku? … [1] 6 Tunajuaje kwamba mwandishi anathamini kazi ya Wambui? … [1] [Jumla: 8]

Question paper, page 4

4 0262/01/M/J/21 © UCLES 2021 Zoezi 2 Wanafunzi wanne wanaelezea kuhusu shughuli watakazozifanya wakati wa likizo. A Juma Nina ujuzi mkubwa sana katika sekta ya teknolojia. Hasa teknolojia ya kompyuta na mitandao. Nilipokuwa mtoto nilipenda sana kucheza michezo mbalimbali kwenye kompyuta. Halafu, polepole nilianza kujaribu kuelewa jinsi michezo hiyo ilivyotengenezwa na niliweza kugundua mengi. Nchi nyingi za Afrika zinathamini matumizi ya kompyuta mashuleni na pia kuendesha shughuli tofauti kama biashara lakini huwa zaidi mijini na si vijijini. Ninadhani ni muhimu kwa wataalamu kutembelea sehemu tofauti na kusambaza ujuzi wa teknolojia ya kompyuta ili watu wote barani humu wafaidike na wafurahie mengi yanayovumbuliwa katika nyanja hii. Ndoto yangu hasa ni kuwafundisha wananchi mbalimbali yote niyajuayo ili na wao waweze kuwa na maendeleo. Likizo hii nitaanza kwa kutoa mafunzo kijijini kwetu. B Luka Nimesoma masomo ya Siasa na Historia za nchi za Kiafrika kwa miaka miwili sasa. Umebaki mwaka mmoja tu wa masomo kabla ya kuhitimu. Bila shaka nitafunzwa mengi zaidi kuhusu serikali na sera tofauti, ingawa hivi sasa akili yangu imechoka kabisa. Nina hamu kubwa ya kupumzika na kutosoma chochote kabisa. Ningependa kuona nchi mbalimbali ambazo sijawahi kuzitembelea. Kwanza kabisa nina hamu ya kuenda Uchina na kuona jinsi watu wanavyoishi huko. Ninavutiwa sana na mila na desturi zao. Ningependa pia kuenda Brazil kwa sababu ninapenda sana mpira wa miguu na ninafikiri nchi hiyo ina wachezaji wazuri sana. Kuenda huko itakuwa ghali sana, kwa hivyo nitatafuta kazi kwenye kampuni ya teknolojia ya simu za kisasa itakayoniwezesha kujinunulia tiketi ya ndege. C Roza Ninasoma masomo ya Utabibu na ninategemea kuwa daktari wa watoto baada ya miaka michache. Mwaka huu itabidi nifanye kazi ya udaktari hapa nchini au nchi yoyote ya jirani. Ningeweza kuajiriwa kwenye hospitali ambapo wazazi wangu ni wauguzi, lakini nilifanya hivyo mwaka uliopita. Mwaka huu ningependelea kuenda Uganda. Huko nitaweza kutoa msaada kwenye magonjwa yanayotishia afya za wengi. Ninadhani malaria ni ugonjwa ambao umekuwa tatizo kwa muda mrefu sana kote barani Afrika, ingawa wengi huuona kama wa kawaida tu. Pia, kwa bahati mbaya, ingawa maendeleo mengi ya kiteknolojia yamefanyika na yameweza kusaidia uelewa wa ugonjwa huu, bado ni tatizo kubwa sana, hasa kwa watoto. Hata kama siwezi kubadili sera mimi mwenyewe, ningetaka kuuona ugonjwa huu ukipotea kabisa. Ninadhani watu wengi hufanya kosa la kutokuutilia maanani kama inavyotakiwa. D Safia Mimi ninasoma masomo ya Isimu ingawa ninavutiwa sana na siasa. Baada ya masomo yangu ningependa kuwa na nafasi nyeti katika uundwaji wa sera zitakazoleta maendeleo nchini kwetu. Kwa mfano, bado nchi yetu ina tatizo kubwa la ugonjwa wa UKIMWI. Kwa kweli, kama ningekuwa mwanasiasa leo hii, ningetoa kipau mbele kikubwa kwenye kuwasomesha wananchi wote kuhusu mambo yote yanayosababisha ugonjwa huu. Hii ingeipa serikali uwezo wa kubadili mawazo ya wananchi kuhusu maradhi haya. Mimi ninafikiri wanasiasa wa leo wanafikiria zaidi masuala ya uchumi. Likizo hii nina mpango wa kutafuta kazi kwenye kituo cha afya na kuelewa sera za nchi kuhusu magonjwa tofauti. Nina hamu hasa ya kuzungumza na wagonjwa wenyewe ili kuelewa ugonjwa huu unavyowaathiri. Wazazi wangu wamejaribu kunishauri nisafiri nao ili kustarehe nao lakini hawajafanikiwa kabisa. Wao wataenda likizo huko Msumbiji kwa mwezi mmoja.

Question paper, page 5

5 0262/01/M/J/21 © UCLES 2021 [Turn over Soma taarifa (7–15) zifuatazo. Weka alama ya tiki (✓) kwenye kisanduku kuonyesha aya (A–D) inayohusiana na kila taarifa. Kuna mfano mmoja hapa chini. Mfano Mwanafunzi yupi ... ana ujuzi mkubwa wa teknolojia ya kompyuta? A ✓ B C D 7 anataka kusafiri ili kustarehe? A B C D [1] 8 ana mpango wa kusomesha? A B C D [1] 9 atahitaji ajira ili kuweza kusafiri? A B C D [1] 10 atakataa nafasi ya kubaki na kufanya kazi nchini kwao? A B C D [1] 11 anataka kubadili sera rasmi za afya? A B C D [1] 12 atajishughulisha na kazi isiyohusiana na masomo yake? A B C D [1] 13 anafikiri kutofahamu teknolojia kunapunguza maendeleo? A B C D [1]

Question paper, page 6

6 0262/01/M/J/21 © UCLES 2021 14 ameweza kutoshawishika na wazazi wake? A B C D [1] 15 anathamini tamaduni tofauti? A B C D [1] [Jumla: 9]

Question paper, page 7

7 0262/01/M/J/21 © UCLES 2021 [Turn over BLANK PAGE

Question paper, page 8

8 0262/01/M/J/21 © UCLES 2021 Zoezi 3 Soma makala yafuatayo kuhusu ndege zisizo na rubani. Huonekana kama vidude vya kuchezea na ni marufuku katika mbuga kadhaa za wanyama kwa sababu ya sauti yake ya kukera ifananayo na nyuki. Hata hivyo, ndege zisizo na rubani zimeanza kuwa jambo la kawaida katika maisha ya kila siku. Hurushwa kutoka mbali kwa kutumia kifaa ardhini kinachoshikwa na mtu. Pia huweza kufika sehemu zisizofikika kirahisi. Kwa hivyo, ni chombo muhimu kwa mashirika mengi, ingawa huleta changamoto. Ndege zisizo na rubani zinaweza kutumiwa kutafuta vyanzo vya maji chini ya ardhi na kuchunguza afya ya mazao. Ili kufanya hivyo, zinahitaji kupaa zikiwa karibu na ardhi huku zikipiga picha. Hata hivyo, mara nyingi huruka juu ya watu ambao hawajashauriwa na inawezekana hawajakubaliana na uwepo wao. Jambo hili linaweza kuwa na athari mbaya kwa jamii zile zile ambazo ndege zisizo na rubani zinataka kusaidia. Mtu mmoja anayefanyia uchunguzi jambo hili ni Profesa Muturi Njeri. Anasema ‘uonekano wa ndege hizi unaweza kuleta tuhuma na wasiwasi kama watu hawajashauriwa tangu hapo awali. Watu wanazihusisha na jeshi hivyo huogopa namna ambavyo mamlaka husika yanavyoweza kuzitumia’. Njeri anatoa mfano wa kuhifadhi misitu, ambapo ndege zisizo na rubani zinaweza kuchunguza afya ya wanyama pori na miti. Utafiti wake unaonyesha kwamba wenyeji hawataki kuingia porini wanapofahamu uwepo wa ndege hizo. Hii ni kwa sababu wao hupata hofu, hata kama wakiwa hawafanyi jambo baya. Pia kumekuwa na ripoti za ndege hizi kuharibiwa na kudunguliwa. Matumizi salama Hata hivyo, matumizi ya ndege zisizo na rubani yanazidi kukua jinsi zinavyoendelea kuwa madhubuti na kuwa na kazi tofauti. Kwa mfano, hivi karibuni Shirika la Kimataifa la Elimu na Watoto limeanza kutuma dawa nchini Malawi kwa kuzitimia. Serikali ya Afrika Kusini inazitumia kusaka majangili misituni, wakati nchi nyingi zinafuatilia hali ya barabara mashambani kwa kutumia picha zake. Khalid Kumbuka ni mkuu wa shirika lililopo Afrika Mashariki linalowapa wateja wao, kama wakulima na wafanya biashara, picha za viwanja vyao kutoka hewani. Amejionea mwenyewe athari chanya za ndege zisizo na rubani. Mwaka 2015, aliongoza timu yake katika mradi wa kuwaonyesha wakulima waliokuwa majirani ukubwa na mipangilio ya mashamba yao. ‘Wakulima waliopokea picha hizo waliweza kutambua maeneo yenye nafasi za ziada ili kulima zaidi. Kwa hivyo, uzalishaji uliongezeka,’ alieleza bwana Kumbuka. ‘Zaidi ya hapo, wakulima wengi walifurahia picha hizo na kuzitundika ukutani ndani ya nyumba zao.’ Anasema kwamba timu yake hushauriana na jamii tofauti kabla ya kutumia ndege zisizo na rubani, hata kama tayari wana kibali cha serikali. ‘Kufuatana na hayo, hatujawahi kuona kesi ambapo watu wameleta mashitaka. Kwa kawaida watu hufurahi. Wanazielewa faida na kwamba ndege inayopiga picha hufanya hivyo kwa salama.’ Matumizi salama hayahusu kushauriana na jamii tu. Pia yanahusu data gani zinakusanywa na jinsi zinavyotumika, hasa tukizingatia kwamba ndege zisizo na rubani zina uwezo wa kupiga picha nzuri sana za watu na kukusanya data nyeti. Kanuni za maadili Serikali zinafahamu hatari zinazoweza kujitokeza. Mwaka huu, nchi 42 zilikubali kuendeleza viwango vya kimataifa vya kutunza na kulinda data. Hata hivyo, sheria zinaweza kutekelezwa vibaya ndani ya nchi na hubadilika kati ya nchi tofauti. Hivi karibuni, Kenya imepiga marufuku ndege zisizo na rubani,

Question paper, page 9

9 0262/01/M/J/21 © UCLES 2021 [Turn over ingawa nchi nyingine zinaziruhusu kwa ada za juu. Licha ya hayo, Njeri bado ana matumaini, kwa sababu uwepo wa sheria tofauti ni bora kuliko kutokuwa na sheria zozote. Njeri anataka wanaofanya utafiti wawajibike zaidi, kwa mfano kwa kutunza na kulinda data vizuri zaidi. ‘Nini kitatokea kama mtafiti akipiga picha ya shughuli haramu, au kama unapata video ya mtu anawinda tembo? Je, utaenda kushitaki polisi au utaifuta? Matatizo haya yanatakiwa yashughulikiwe mapema kwa kutumia kanuni na sera wazi.’ Kwa bwana Kumbuka, mpangilio ni muhimu kwa sifa nzuri ya kampuni yake. Mifano ya sera zao ni pamoja na kukataa kutoa picha zinazowatambulisha watu na shughuli zao. Anaamini kwamba mashirika mengi zaidi yanafuata mfano wao, ingawa bado kuna safari ndefu. Andika maelezo mafupi chini ya vichwa vya habari (16–18) vinavyotokana na makala uliyoyasoma. 16 Matumizi makuu ya ndege zisizo na rubani: • … • … • … [3] 17 Mabadiliko ya vitendo vya wenyeji tofauti kuhusu ndege zisizo na rubani: • … • … • … [3] 18 Maoni ya Njeri kuhusu ndege zisizo na rubani: • … • … • … [3] [Jumla: 9] Katika zoezi 4, utatumia maelezo haya kutunga ufupisho.

Question paper, page 10

10 0262/01/M/J/21 © UCLES 2021 Zoezi 4 Makala ya zoezi 3 yanazungumzia matumizi ya ndege zisizo na rubani. 19 Sasa tunga ufupisho wa faida na hasara za ndege zisizo na rubani. Unaweza kutumia maelezo yako mengine kutoka zoezi 3 ili kukusaidia. Ufupisho wako usizidi maneno 100. Tumia maneno yako mwenyewe kadiri iwezekanavyo. Utapata alama zisizozidi 4 kwa maudhui ya ufupisho wako, na alama zisizozidi 6 kwa lugha makini na sahihi. … … … … … … … … … … … … … … [Jumla: 10]

Question paper, page 11

11 0262/01/M/J/21 © UCLES 2021 [Turn over Zoezi 5 20 Mwandikie barua pepe rafiki yako anayeishi nje ya nchi kuhusu shule yako. Unapaswa kutaja: • Shule yako ikoje • Unapenda nini kuhusu shule yako • Ungebadilisha nini shuleni kwako Barua pepe yako isizidi maneno 120. Utapata alama zisizozidi 3 kwa maudhui ya barua yako, na alama zisizozidi 5 kwa mtindo na umakini wa matumizi ya lugha yako. … … … … … … … … … … … … … … [Jumla: 8]

Question paper, page 12

12 0262/01/M/J/21 © UCLES 2021 Zoezi 6 21 ‘Vinywaji vyenye sukari nyingi ni tatizo kubwa kwa afya ya vijana duniani.’ Je, unakubaliana na wazo hili? Andika makala katika gazeti la shule ili kutoa maoni yako. Makala yasizidi maneno 200. Matumizi mazuri ya sukari ni starehe maishani! Kuna matatizo makubwa zaidi kama uvutaji wa sigara ambao una athari mbaya zaidi kwa afya. Unaweza kutumia maoni ya hapo juu, na pia ni lazima kutumia mawazo yako mwenyewe. Utapata alama zisizozidi 8 kwa maudhui ya makala, na alama zisizozidi 8 kwa mtindo na umakini wa matumizi ya lugha yako. … … … … … … … … … … … … … … … … …

Question paper, page 13

13 0262/01/M/J/21 © UCLES 2021 … … … … … … … … … … … … … [Jumla: 16]

Question paper, page 14

14 0262/01/M/J/21 © UCLES 2021 BLANK PAGE

Question paper, page 15

15 0262/01/M/J/21 © UCLES 2021 BLANK PAGE

Question paper, page 16

16 0262/01/M/J/21 © UCLES 2021 Permission to reproduce items where third-party owned material protected by copyright is included has been sought and cleared where possible. Every reasonable effort has been made by the publisher (UCLES) to trace copyright holders, but if any items requiring clearance have unwittingly been included, the publisher will be pleased to make amends at the earliest possible opportunity. To avoid the issue of disclosure of answer-related information to candidates, all copyright acknowledgements are reproduced online in the Cambridge Assessment International Education Copyright Acknowledgements Booklet. This is produced for each series of examinations and is freely available to download at www.cambridgeinternational.org after the live examination series. Cambridge Assessment International Education is part of the Cambridge Assessment Group. Cambridge Assessment is the brand name of the University of Cambridge Local Examinations Syndicate (UCLES), which itself is a department of the University of Cambridge. BLANK PAGE