Cambridge IGCSE Swahili 0262 — 2023 May/June Paper 1 · Variant 0

0262/10/M/J/23 · 60 marks · ≈68 min

The question paper and its mark scheme, free to read here and free to download. This is Cambridge’s own paper, exactly as it was sat.

Question paper16 pages

Cambridge IGCSE Swahili 0262 2023 May/June Paper 1 · Variant 0 question paper, page 1 of 16
Page 1 of 16
Cambridge IGCSE Swahili 0262 2023 May/June Paper 1 · Variant 0 question paper, page 2 of 16
Page 2 of 16
Cambridge IGCSE Swahili 0262 2023 May/June Paper 1 · Variant 0 question paper, page 3 of 16
Page 3 of 16
Cambridge IGCSE Swahili 0262 2023 May/June Paper 1 · Variant 0 question paper, page 4 of 16
Page 4 of 16
Cambridge IGCSE Swahili 0262 2023 May/June Paper 1 · Variant 0 question paper, page 5 of 16
Page 5 of 16
Cambridge IGCSE Swahili 0262 2023 May/June Paper 1 · Variant 0 question paper, page 6 of 16
Page 6 of 16
Cambridge IGCSE Swahili 0262 2023 May/June Paper 1 · Variant 0 question paper, page 7 of 16
Page 7 of 16
Cambridge IGCSE Swahili 0262 2023 May/June Paper 1 · Variant 0 question paper, page 8 of 16
Page 8 of 16
Cambridge IGCSE Swahili 0262 2023 May/June Paper 1 · Variant 0 question paper, page 9 of 16
Page 9 of 16
Cambridge IGCSE Swahili 0262 2023 May/June Paper 1 · Variant 0 question paper, page 10 of 16
Page 10 of 16
Cambridge IGCSE Swahili 0262 2023 May/June Paper 1 · Variant 0 question paper, page 11 of 16
Page 11 of 16
Cambridge IGCSE Swahili 0262 2023 May/June Paper 1 · Variant 0 question paper, page 12 of 16
Page 12 of 16
Cambridge IGCSE Swahili 0262 2023 May/June Paper 1 · Variant 0 question paper, page 13 of 16
Page 13 of 16
Cambridge IGCSE Swahili 0262 2023 May/June Paper 1 · Variant 0 question paper, page 14 of 16
Page 14 of 16
Cambridge IGCSE Swahili 0262 2023 May/June Paper 1 · Variant 0 question paper, page 15 of 16
Page 15 of 16
Cambridge IGCSE Swahili 0262 2023 May/June Paper 1 · Variant 0 question paper, page 16 of 16
Page 16 of 16

Mark scheme

No mark scheme is in the library for this paper.

Paper as text

Question paper, page 1

This document has 16 pages. Any blank pages are indicated. [Turn over Cambridge IGCSE™ SWAHILI 0262/01 Paper 1 Reading and Writing May/June 2023 2 hours You must answer on the question paper. No additional materials are needed. INSTRUCTIONS ● Answer all questions. ● Use a black or dark blue pen. ● Write your name, centre number and candidate number in the boxes at the top of the page. ● Write your answer to each question in the space provided. ● Do not use an erasable pen or correction fluid. ● Do not write on any bar codes. ● Dictionaries are not allowed. INFORMATION ● The total mark for this paper is 60. ● The number of marks for each question or part question is shown in brackets [ ]. * 4 0 1 2 2 5 4 8 6 0 * DC (CJ) 319194/3 © UCLES 2023

Question paper, page 2

2 0262/01/M/J/23 © UCLES 2023 Zoezi 1 Soma kifungu kifuatacho kuhusu vijana na mazingira halafu jibu maswali yanayofuata. Mara ya kwanza kumsikia Vanessa Nakate ilikuwa mwaka uliopita. Alitembelea shule moja kijijini kwetu na kutuambia kwamba angerudi baada ya muda mfupi na kutujengea majiko makubwa yatakayotumia nishati mbadala kupika chakula. Majiko hayo yangetumia miale ya jua. Alitueleza kwamba yeye alishasaidia shule chache kutokana na ufadhili ambao huupata sehemu tofauti. Baada ya muda mfupi, Vanessa alirudi na akajenga hayo majiko. Alitufahamisha kwamba, yale majiko ya kuni na mkaa tuliyokuwa tukiyatumia pale awali yalikuwa ni chanzo kikuu cha uchafuzi wa mazingira. Mimi binafsi nilishasoma shuleni kwamba ukataji wa miti ili kupata kuni za kupikia, hasa ule ukataji usiodhibitiwa, ni tishio kubwa kwa uwepo wa misitu. Na kama tujuavyo misitu ni muhimu sana kuendeleza mifumo ya maisha yetu sisi binadamu, maisha ya wanyama na pia mimea. Hivyo nilielewa kwamba alilofanya Vanessa Nakate lilikuwa jambo la muhimu sana. Vanessa alisema kwamba ni lazima vijana wa Kiafrika washiriki katika majadiliano ya kimataifa yanayohusu mazingira. Ili binadamu waweze kuishi maisha bora, ninadhani kuna umuhimu kwetu kuhifadhi mazingira. Mara nyingi baada ya makongamano na mazungumzo ya kimataifa, vijana husikilizwa. Mashirika tofauti huamini uongozi wa vijana duniani ni suluhisho na huwapa pesa kwa miradi. Kwa njia hii, Vanessa aliweza kuanzisha kazi yake na kupambana na changamoto za mazingira. Vanessa Nakate alizaliwa Uganda na alihitimu chuo kikuu cha Makerere akiwa na shahada ya masomo ya Biashara. Alianza kuwa mwanaharakati wa mazingira mwaka 2019 baada ya kuona vijana duniani wakijulikana kwa kuandamana huku wakikumbusha serikali zao kuchukua hatua zitakazoleta mabadiliko ya kimazingira duniani. Vanessa alifanya hivyo pia. Alianza kwa kuwaomba ndugu zake waende naye sehemu tofauti katika jiji la Kampala huku wakiwa wamebeba mabango. Mabango waliyobeba yalikuwa na maneno kama ‘mazingira ni uhai’, ‘gomea hali ya hewa’ na ‘ukipanda mti, unapanda msitu’. Wapita njia na madereva waliwashangaa. Yeye alihisi kwamba ameweza kuongeza sauti yake kwenye mazungumzo yanayohusu mazingira. Ndugu zake waliporudi shuleni yeye aliendelea kusimama nje ya ofisi tofauti za serikali peke yake huku akipigania kusikilizwa. Aliwasaka wabunge na kuwataka wabadili sera za uwekezaji. Vanessa alitaka serikali ikabiliane na viwango vya maji katika Ziwa Viktoria ambavyo vimekuwa vikipanda na kuleta hatari ya mafuriko. Mwishoni mwa mwaka 2019 Vanessa alianza kutambulika na kualikwa kwenye vyombo vya habari na mikutano tofauti duniani. Anasema kwamba, ‘sehemu kubwa ya dunia haina furaha kwa sababu ya mgogoro wa hali ya hewa, ninataka kuona watu wenye furaha na dunia yenye furaha’.

Question paper, page 3

3 0262/01/M/J/23 © UCLES 2023 [Turn over 1 Vanessa Nakate aliahidi kujenga nini? … [1] 2 Kijiji kilikuwa kinafanya matendo gani ambayo ni mabaya kwa mazingira? Taja matendo mawili. … … [2] 3 Taja mawazo ya mwandishi kuhusu uboreshaji wa maisha kiujumla. … [1] 4 Imani gani ilimsaidia Vanessa kuanzisha mradi wake? … [1] 5 Jambo gani lilimfanya Vanessa aanze kutambulika kama mwanaharakati? … [1] 6 Tunajuaje kwamba Vanessa hakukata tamaa? Taja sababu mbili. … … [2] [Jumla: 8]

Question paper, page 4

4 0262/01/M/J/23 © UCLES 2023 Zoezi 2 Wanafunzi wanne wanaelezea kuhusu maisha yao. A Roza Mimi nimezaliwa mji unaoitwa Ujiji. Mji huo huitwa mwisho wa reli kwa sababu ujenzi wa reli uliishia hapo. Nilipokuwa na miaka kumi na sita, baba yangu alipata uhamisho wa kazi na mimi na familia yangu tulihamia katika jiji la Dar es Salaam. Mwanzoni niliona tabu sana kuwa hapo kwani sikuwa na rafiki yeyote na pia sikupenda joto la jijini hapo. Pia nilipokuwa shuleni, wenzangu walinitania kwani nilipozungumza nilikuwa na lafudhi tofauti. Lakini baada ya muda nilizoea maisha ya mjini na nilipata kazi ya kuuza tiketi za treni katika stesheni ya reli. Mojawapo ya marupurupu ya kazi yangu ni uwezo wa kusafiri kuenda popote pale kwa kutumia reli. Mara kwa mara mimi huenda Ujiji kuwatembelea ndugu, jamaa na rafiki zangu. B Mikeli Wazazi wangu walikuwa wafugaji wa ng’ombe, ngamia na mbuzi na hivi leo, mimi pia nimerithi kazi yao. Sisi tuna shamba kubwa sana na tumeishi hapa Arusha maisha yetu yote. Sidhani kama tutahama. Hali ya hewa hapa ni nzuri kwa wanyama na pia kuna madaktari wazuri kwa wanyama wetu. Nilipokuwa mdogo nilipata ajali wakati wa kuingiza ng’ombe zizini na tangu wakati huo nimekuwa nikitembea kwa kutumia fimbo inayonisaidia. Baada tu ya ajali hiyo nilitaka mguu wa bandia kwani nilifikiri wenzangu wangenitania kwa kuwa na kilema cha mguu. Kwa bahati nzuri, haikuwa hivyo. Wenzangu walinionyesha mapenzi na nimeishi maisha mazuri tu. Mwaka uliopita nilijiunga na wafugaji wengine na tulipanda mlima Kilimanjaro. Kati ya waliopanda mlima walikuwepo waliotoka Dar es Salaam na miji mingine. Nilifurahi kuona watu si wavivu wa kusafiri na wanakubali kuenda masafa marefu ili kuwa na wenzao. C Micha Ninaishi Nairobi pamoja na mama yangu, ingawa nilizaliwa Mombasa ambapo joto lilinikera sana. Mimi ni mtoto pekee na mama yangu amehangaika maisha yake yote kunipeleka kwenye shule nzuri na kunipa maisha bora. Nina tatizo kubwa ambalo sijui jinsi ya kulishughulikia. Mimi sipendi kufanya kazi nzito na pia sipendi kufanya chochote kwa muda mrefu. Mama yangu anasema kwamba nimekuwa hivi tangu nilipokuwa mtoto. Walimu wangu walihisi mimi ninadekezwa na mama. Ukweli ni kwamba, bado sijapata kitu kitakachonisisimua ili niwache tabia hii. Ninapenda sana wanyama, hasa paka wangu aliyezoea kujilaza jikoni kwangu. Ningeweza kuwa daktari wa wanyama lakini bila shaka ingebidi kuwatibu wanyama wakubwa kama ng’ombe na ngamia ambao hawanivutii kabisa. Pia sijasomea masomo ya sayansi na wala sitafuti kazi. Bado ninataka muda wa kuchagua ajira ingawa kwanza nitasafiri kuona dunia. D Farhiya Maisha yangu yote nimeishi kwingi na nimekuwa na ndoto ya kuishi Ulaya, kwa sababu nilidhani kule hakuna joto kama huku kwetu. Baba yangu ambaye amewahi kuishi na kufanya kazi huko aliniambia kuwa wakati wa kiangazi Ulaya huwa na joto linalochoma sana. Mimi siwezi kuamini hadi pale nitakapojionea mwenyewe. Kama ningekuwa na kazi kwenye sehemu kubwa kama stesheni ya reli ningesikia raha kupulizwa na kiyoyozi siku nzima. Tena, kwa vile hivi sasa nipo mbioni kutafuta kazi, itanibidi kupatembelea huko. Mimi ninazungumza lugha nyingi kwa hivyo ningeweza kuwa mwongoza watalii Kilimanjaro. Jambo lingine ni kuwa, mimi ninapenda maisha ya shamba, ningeweza kufuga wanyama kama kuku na mbuzi na kuwauza. Kwa kweli nina mawazo mengi kuhusu maisha yangu lakini bado sijafanya maamuzi.

Question paper, page 5

5 0262/01/M/J/23 © UCLES 2023 [Turn over Soma taarifa (7–15) zifuatazo. Weka alama ya tiki (✓) kwenye kisanduku kuonyesha aya (A–D) inayohusiana na kila taarifa. Kuna mfano mmoja hapa chini. Mfano Nani … alizaliwa mwisho wa reli? A ✓ B C D 7 anaishi mahali alipozaliwa? A B C D [1] 8 ana tabia ya uvivu? A B C D [1] 9 alitaniwa alipokuwa mdogo? A B C D [1] 10 angependa kuhama kwa sababu ya hali ya hewa? A B C D [1] 11 anafanya kazi katika sekta ya usafiri? A B C D [1] 12 anatafuta ajira? A B C D [1] 13 alionyeshwa thamani ya urafiki utotoni? A B C D [1]

Question paper, page 6

6 0262/01/M/J/23 © UCLES 2023 14 anafanya kazi kama ya wazazi wake? A B C D [1] 15 anaishi na mnyama mpendwa? A B C D [1] [Jumla: 9]

Question paper, page 7

7 0262/01/M/J/23 © UCLES 2023 [Turn over BLANK PAGE PLEASE TURN OVER FOR EXERCISE 3

Question paper, page 8

8 0262/01/M/J/23 © UCLES 2023 Zoezi 3 Soma makala yafuatayo kuhusu safari za angani. Kumekuwa na mazungumzo mengi kuhusu utalii wa safari za anga. Kwa miaka mingi wanasayansi wamekuwa wakienda huko na kurudi. Pia roboti tofauti zimekuwa zikitumwa angani ili kufanya uchunguzi wa kisayansi unaotusaidia kuielewa dunia. Lakini hivi karibuni, mambo yameanza kubadilika baada ya wadau wachache kuamua kwamba wangependa kuwekeza fedha kwenye miradi itakayowawezesha watu wa kawaida kuenda kutembea angani na kuona maajabu yaliyopo huko mbinguni. Mtu wa kawaida wa kwanza kutembelea anga alikuwa mfanyabiashara mmoja aliyekwenda huko mwaka 2001. Alilipia maelfu ya fedha za kigeni ili kufanya hivyo. Sasa makampuni binafsi yameanza kulifanyia mchakato suala zima la watu kuenda angani. Kampuni zinazojulikana zaidi ni Dunia Duara na Chanzo cha Maisha. Kampuni hizi zinamilikiwa na wafanyabiashara matajiri. Dunia Duara inamilikiwa na Juma Hamisi wakati Chanzo cha Maisha ni mali ya Roza Mahiri. Tofauti kati yao ni kuwa wengi wanaamini kwamba Juma Hamisi ana uthubutu zaidi ya Roza Mahiri. Pia Juma Hamisi anatumia watu kudhamini mradi wake wa anga. Roza Mahiri anatumia pesa zake mwenyewe na anaamini kwamba polepole ndiyo mwendo, hataki kuuharakisha mradi wake wa anga ingawa anataka kuwa na nafasi katika historia ya dunia ya kuwezesha utalii wa anga. Kwa miaka michache sasa, Roza Mahiri amekuwa akiwekeza mamilioni ya pesa kwenye ujenzi wa roketi ambayo itakuwa na uwezo wa kuwapeleka watu sita angani. Roketi hiyo itapaa kilometa 100 kutoka ardhini hadi angani. Safari ya kwanza ya roketi hiyo imeshapangwa. Wasafiri ni yeye mwenyewe, kaka yake na mdau mmoja aliyebahatika kushinda mnada wa tiketi ya kuenda huko. Mdau huyo atalipia mamilioni ya pesa za kigeni ili kupata nafasi ya kuenda huko. Roza Mahiri amekuwa na hamu ya kutalii anga tangu utotoni mwake. Ninafikiri kwa miaka nenda, miaka rudi, amekuwa akijiuliza, je angani kukoje na je atahisi vipi pale atakapokuwa sehemu ambayo haina mvuto wa ardhi na kuweza kuelea hewani. Nilisoma kwamba yeye alianza kujiuliza maswali kuhusu anga alipokuwa na miaka mitano baada ya kuona kwenye televisheni roketi zikivurumisha vumbi kubwa kabla ya kupaa angani. Ninadhani kabla ya roketi kupaa, ni lazima wahusika wahakikishe kwamba hakuna mtu yeyote karibu ili kuwe na usalama. Roketi atakayoitumia Roza imefanya majaribio 15 ya kuenda angani na kurudi. Hakuna binadamu aliyewahi kusafiri na roketi hiyo; wakati wa majaribio mwanasesere alipakizwa ndani ya roketi ili kuona usalama wa safari. Mwanasesere huyo alirudi ardhini akiwa mzima kabisa na wala hakusogea kutoka pale alipowekwa kabla ya safari. Kwa kweli safari ya kuenda angani inasisimua sana. Bila shaka mtu ataweza kuona nyota na kuiona dunia ikiwa kama mpira kutoka angani. Lakini roketi zinazokwenda huko husafiri umbali mrefu kwa muda mfupi sana hivyo huhitaji kuunguza mafuta mengi yenye thamani ya juu ili kuweza kusafiri kwa mwendo wenye kasi kubwa. Upaaji wake ni wa njia maalumu kwani roketi huruka zikiwa wima. Hii ndiyo maana watu ndani ya roketi hufunga mikanda na kukaa kwa utulivu ili wasiumie. Swali ninalojiuliza kwa muda sasa ni je, pale hizi safari zitakapoweza kufanywa na watu wa kawaida, nani atapenda kuenda na nani ataweza kuenda? Kwa upande mmoja, pesa nyingi zinahitajika kwa safari hiyo. Kwa hivyo, ni watu wanaojiweza kifedha tu ambao wataweza kuenda. Hii inamaanisha kwamba tofauti kati ya watu duniani zitazidi kuwa kubwa. Lakini pia, mtu akibahatika kwenda, ataona maajabu ya anga na dunia; jambo ambalo hatasahau milele.

Question paper, page 9

9 0262/01/M/J/23 © UCLES 2023 [Turn over Andika maelezo mafupi chini ya vichwa vya habari (16–18) vinavyotokana na makala uliyoyasoma. [Jumla: 9] Katika zoezi 4, utatumia maelezo haya kutunga ufupisho. 16 Sababu zilizomfanya Roza Mahiri kuwekeza kwenye utalii wa anga: • … • … • … [3] 17 Ushahidi wa usalama kuwa jambo muhimu kwenye safari za anga: • … • … • … [3] 18 Unajuaje kwamba uchumi una nafasi kubwa kwenye utalii wa anga? • … • … • … [3]

Question paper, page 10

10 0262/01/M/J/23 © UCLES 2023 Zoezi 4 Makala ya zoezi 3 yanazungumzia safari za angani. 19 Sasa tunga ufupisho unaoonyesha faida na hasara za safari za kutalii anga. Unaweza kutumia maelezo yako mengine kutoka zoezi 3 ili kukusaidia. Ufupisho wako usizidi maneno 100. Tumia maneno yako mwenyewe kadiri iwezekanavyo. Utapata alama zisizozidi 4 kwa maudhui ya ufupisho wako, na alama zisizozidi 6 kwa lugha makini na sahihi. … … … … … … … … … … … … … … [Jumla: 10]

Question paper, page 11

11 0262/01/M/J/23 © UCLES 2023 [Turn over Zoezi 5 20 Umepata nafasi ya kutoa maelezo kuhusu urafiki. Andika blogu itakayosomwa na watu duniani pote. Unapaswa kutaja: • rafiki yako mpenzi • shughuli unazopenda kufanya na rafiki zako • changamoto za urafiki. Blogu yako isizidi maneno 120. Utapata alama zisizozidi 3 kwa maudhui ya blogu yako, na alama zisizozidi 5 kwa mtindo na umakini wa matumizi ya lugha yako. … … … … … … … … … … … … … … [Jumla: 8]

Question paper, page 12

12 0262/01/M/J/23 © UCLES 2023 Zoezi 6 21 ‘Pesa ndiyo chanzo cha matatizo duniani’. Je, unakubaliana na wazo hili? Andika makala katika gazeti la shule ili kutoa maoni yako. Makala yasizidi maneno 200. Vitu muhimu duniani, kwa mfano mapenzi, huwa bure! Pesa ndio ufunguo wa maisha. Lazima kuwa na pesa ili uwe na furaha. Unaweza kutumia maoni ya hapo juu, na pia ni lazima kutumia mawazo yako mwenyewe. Utapata alama zisizozidi 8 kwa maudhui ya makala, na alama zisizozidi 8 kwa mtindo na umakini wa matumizi ya lugha yako. … … … … … … … … … … … … … … … … … …

Question paper, page 13

13 0262/01/M/J/23 © UCLES 2023 … … … … … … … … … … … … [Jumla: 16]

Question paper, page 14

14 0262/01/M/J/23 © UCLES 2023 BLANK PAGE

Question paper, page 15

15 0262/01/M/J/23 © UCLES 2023 BLANK PAGE

Question paper, page 16

16 0262/01/M/J/23 © UCLES 2023 Permission to reproduce items where third-party owned material protected by copyright is included has been sought and cleared where possible. Every reasonable effort has been made by the publisher (UCLES) to trace copyright holders, but if any items requiring clearance have unwittingly been included, the publisher will be pleased to make amends at the earliest possible opportunity. To avoid the issue of disclosure of answer-related information to candidates, all copyright acknowledgements are reproduced online in the Cambridge Assessment International Education Copyright Acknowledgements Booklet. This is produced for each series of examinations and is freely available to download at www.cambridgeinternational.org after the live examination series. Cambridge Assessment International Education is part of Cambridge Assessment. Cambridge Assessment is the brand name of the University of Cambridge Local Examinations Syndicate (UCLES), which is a department of the University of Cambridge. BLANK PAGE

What you needed in this session

Cambridge’s own grade thresholds for 2023 May/June, Paper 1 · Variant 0. A higher threshold means an easier paper — the bar moves with how the cohort did.

A41/60
B36/60
C30/60
D25/60
E20/60
F15/60
G10/60